Jumapili 11 Oktoba 2026 - 22:50
Watu wote washike kalamu ili kumtambulisha Imamu Shahidi na Sayyid Hassan Nasrullah

Ayatullah Najmuddin Tabasi, akisisitiza umuhimu wa kutambulisha vipengele mbalimbali vya utu na fikra za Imamu Khamenei Shahidi na Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, alisema: “Kila mmoja anapaswa kushika kalamu kwa ajili ya kuwatambulisha viongozi hawa wawili wakubwa na kufafanua misimamo yao, kazi zao na huduma zao kwa ajili ya vizazi vijavyo.”

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Najmuddin Tabsi aliyasema hayo katika hafla ya kumuenzi Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Nasrallah (ra), iliyofanyika katika Madrasa ya Kidini ya Alawi, Qum, chini ya anwani isemayo ‘Wa Pekee Katika Historia ya Sham’. Katika hafla hiyo, alizungumzia vipengele mbalimbali vya utu na mapambano ya Katibu Mkuu wa Shahidi wa Hizbullah ya Lebanon, huku akisisitiza umuhimu wa kuhifadhi na kutambulisha urithi wake wa fikra, utamaduni na siasa.

Kila mmoja anapaswa kuandika kwa ajili ya kumtambulisha Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah

Ayatullah Tabsi, akisisitiza umuhimu wa kumtambulisha Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah (ra), alisema: “Ni lazima kushika kalamu kwa ajili ya kumtambulisha mtu huyu wa kipekee, kukusanya misimamo yake, hotuba zake, utendaji wake na vipengele mbalimbali vya utu wake, kisha kuvitambulisha kwa vizazi vijavyo.”

Aliongeza kuwa, kuwatambulisha watu wakubwa wa aina hii haipaswi kuishia katika kuandaa hafla za kumbukumbu za kila mwaka na matukio maalumu pekee, Badala yake ni lazima kuandaa na kuchapisha maandishi na vitabu vyenye kudumu vinavyowahusu, ili vizazi vijavyo viweze kuwafahamu watu hawa mashuhuri.

Sayyid wa Muqawama alikuwa mtiifu kwa Uongozi

Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, akizungumzia namna Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah (ra) alivyokuwa akifuata na kushikamana na Wilaya, alisema: “Shahidi Nasrallah alikuwa na mapenzi na heshima ya pekee kwa Imamu Shahidi (ra), na alikuwa akifuata njia ya Wilaya.”

Alisimulia kumbukumbu moja kuhusu Sayyid Hassan Nasrallah (ra), akisema: “Katika moja ya mikutano ya nchi za Kiislamu iliyofanyika Tehran, baada ya hotuba ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (ra), Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah (ra) alijitokeza kutoka katikati ya umati wa watu na kwenda kumfikia Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, kisha akambusu mkono wake.”

Ayatullah Tabsi aliendelea kusema: “Sayyid Hassan Nasrallah (ra) alikuwa amesema kwamba watu kutoka nchi za Kiarabu na Ulaya walikuwa wakipanga foleni ili kupeana naye mikono na kupiga naye picha. Hata hivyo, yeye alisonga mbele ili aubusu mkono wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (ra), ili dunia ijue kwamba nguvu na uwezo alionao vimetokana na wapi.”

Watu wote washike kalamu ili kumtambulisha Imamu Shahidi na Sayyid Hassan Nasrullah

Nguvu na uwezo wa Shahidi Nasrallah vilitokana na shule ya Imamu Khamenei

Mwalimu wa Hawza ya Qum, huku akisisitiza kwamba Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa akiona nguvu na uwezo wake kuwa vimefungamana na Mapinduzi ya Kiislamu na Wilayat Faqihi, alibainisha kuwa; Sayyid wa Muqawama aliamini kwamba nguvu na uwezo huo aliupata ni kutoka katika shule ya Imamu Khamenei (ra), aidha alikuwa na ufuatiliaji na kujali kwa namna ya pekee masuala ya Iran na Hawza.

Aliongeza kuwa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah (ra) alikuwa akifuatilia kwa karibu masuala yanayohusu Marja'iyya, Hawza na mambo yanayohusiana na Iran. Vilevile, alikuwa akilipa umuhimu wa pekee suala la kushikamana na Wilaya na kudumisha uhusiano na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (ra).

Shahidi Nasrullah aliibadilisha Lebanon

Ayatullah Tabasi, akizungumzia nafasi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah (ra) katika mabadiliko yaliyotokea nchini Lebanon, alisema: “Shughuli za Sayyid wa Muqawama hazikuwa zimewekewa mipaka katika uwanja wa kijeshi pekee, bali mipango mikubwa iliandaliwa pia katika uwanja wa utamaduni, na Hizbullah iliupa umuhimu wa kipekee utekelezaji wa shughuli za kiutamaduni na malezi.”

Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum aliendelea kusema kuwa, miongoni mwa hatua zilizofuatwa katika mwelekeo huo ni kuanzishwa kwa Hawza za na shule, kuwaandaa wahubiri wa dini, kulea na kuandaa wanazuoni, kuwaandaa wasomaji wa kaswida na mashairi ya kidini, pamoja na kuandaa kozi za mafunzo.

Ayatullah Tabasi, akizungumzia shughuli za kiutamaduni za Hizbullah aliongeza kuwa; nchini Lebanon mipango iliandaliwa kwa ajili ya kulea kizazi kipya na kuimarisha utamaduni wa kidini, shule za Al-Mahdi pamoja na vituo vya Hawza na taasisi za kiutamaduni zilianzishwa katika muktadha huo.

Akizungumzia kuenea majlisi za maombolezo nchini Lebanon, alibainisha kuwa; katika kipindi cha uongozi wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah (ra), majlisi za maombolezo ya Aba Abdillah Al-Hussein (as) zilienea zaidi nchini humo. Katika siku za mwezi wa Muharram, eneo la Dhahiyah liligeuka kuwa Husseiniyya kubwa.

Ushawishi wa Shahidi Nasrullah katika harakati za Muqawama

Mwalimu wa Hawza ya Qum, akizungumzia ushawishi wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah (ra) katika harakati za Muqawama, alisema: “Shughuli za Shahidi Nasrallah hazikuishia nchini Lebanon pekee, bali pia zilikuwa na ushawishi katika harakati za Muqawama katika eneo hili.”

Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, huku akizungumzia uhusiano wa Sayyid wa Muqawama na makundi ya Wapalestina aliongeza kuwa; mahusiano hayo ya kiutamaduni na kiitikadi yalisaidia kuimarisha uhusiano kati ya makundi mbalimbali ya Muqawama na utamaduni wa Ahlul-Bayt (as).

Hawza zimekuwa zikisimama dhidi ya maadui siku zote

Mwalimu wa Hawza ya Qum, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, huku akizungumzia historia ya Hawza alisema: “Hawza zimekuwa zikikabiliana na maadui na kuwapinga siku zote. Katika kipindi chote cha historia, wanazuoni wa Kishia wametoa gharama kubwa kwa ajili ya kuilinda dini na madhehebu ya Ahlul-Bayt (as).”

Akizungumzia kuuawa kishahidi, kupelekwa uhamishoni na kufungwa jela wanazuoni wengi katika vipindi mbalimbali vya historia, alisema: “Katika historia ya Hawza, wanazuoni wengi wameuawa kishahidi, huku wengine wakikabiliwa na mashinikizo, kufungwa jela na kupelekwa uhamishoni, hata hivyo Hawza hazikurudi nyuma wala kuiacha njia yao.”

Kitabu Shuhadaa al-Fadhilah, kilichoandikwa na marehemu Allamah Amini (ra), ni miongoni mwa kazi zinazohusu kuwatambulisha wanazuoni waliouawa kishahidi.

Ayatullah Tabasi alisisitiza: “Hawza zimekuwa mstari wa mbele katika harakati za Muqawama siku zote. Wanazuoni na viongozi wa dini wamesimama imara dhidi ya maadui katika nyakati mbalimbali za historia, na pale ilipohitajika, wametoa hata maisha yao katika njia hii.”

Nguvu ya Iran katika vita vya hivi karibuni vilivyolazimishwa ilitokana na mipango madhubuti ya Kiongozi Shahidi

Ayatullah Tabasi, huku akiendelea kuzungumzia vita vya hivi karibuni vilivyolazimishwa na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisema: “Adui alidhani kwamba angeweza kutekeleza nchini Iran mpango unaofanana na ule uliotokea Iraq au Venezuela, lakini tathmini na hesabu zao kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hazikuwa sahihi.”

Mwalimu wa Hawza  ya Qum, akizungumzia matamshi ya Rais wa Marekani kuhusu nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita hivyo vya hivi karibuni, alisema: “Hata Trump mwenyewe alikiri kwamba kama Marekani isingeingia vitani, Israel ingekuwa imeangamizwa.”

Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisisitiza kuwa; nguvu na uwezo huo ni matokeo ya mipango madhubuti iliyowekwa na Kiongozi Shahidi (ra), ambaye alikuwa ameandaa hatua na maandalizi muhimu kabla ya kuuawa kishahidi. Aliongeza kuwa; adui alidhani kwamba kwa kumuua kishahidi Kiongozi huyo angeweza kufikia malengo yake, lakini dhana hiyo haikuwa chochote zaidi ya ndoto isiyokuwa na msingi.

Umuhimu wa kumtambulisha Imamu Shahidi

Ayatullah Tabasi, huku akisisitiza umuhimu wa kutambulisha utu wa Imamu Shahidi (ra) na vipengele mbalimbali vya maisha na shakhsia yake, alipendekeza kwamba: “Ni lazima kushika kalamu kwa ajili ya kumtambulisha Imamu Shahidi na kueleza utu wake, Shahidi Ayatullah al-Udhma Imamu Khamenei (ra) alikuwa mtu adimu na wa kipekee katika zama zetu.”

Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisisitiza kuwa; kazi hii haipaswi kuishia katika kuandaa hafla pekee, badala yake ni lazima kuandika na kuchapisha kazi zenye kudumu zinazomhusu kiongozi huyu, ili vizazi vijavyo vifahamu vipengele mbalimbali vya utu wake na utendaji wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Mwalimu wa masomo ya juu ya elimu ya kidini katika Hawza ya Qum alikumbusha pia: “Vilevile, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa mpiganaji mkubwa Sayyid Hassan Nasrullah, tulikuwa tukishuhudia kwamba kila alipozungumza, maadui walikuwa wakitetemeka kwa hofu. Maneno yake yalikuwa yakiwachochea watu huru duniani kuchukua hatua, na alikuwa akitambuliwa kama shujaa wa Umma wa Kiarabu.

“Je, ushawishi na nguvu hizi zilitokana na kuwa na vifaa na rasilimali nyingi za kimaada? Hapana! Bali, zilitokana na ukweli kwamba alikuwa mwanadamu mwenye imani na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa sababu hiyo, msaada na neema za Mwenyezi Mungu zilikuwa pamoja naye.”

Msimamo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi unatokana na mafundisho na Sunna za Mwenyezi Mungu

Ayatullah Abdullahiy, akihitimisha mazungumzo yake, alisema: “Kwa hiyo, inabainika kwamba maneno na misimamo ya sasa ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu inatokana na mafundisho ya Mwenyezi Mungu na Sunna za Mola. “Sunna hizo zimekuwa zikijidhihirisha wazi katika kipindi chote cha historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na tangu mwanzo wa Uislamu, kupitia harakati za Mtume Mkuu wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), utume wake, harakati ya mapambano ya Ashura na katika vipindi vingine mbalimbali vya historia, aidha uzoefu wetu wa kihistoria unathibitisha ukweli wa mafundisho hayo.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha